Katika kona yake kwenye gazeti la New York Times jana Ijumaa, Friedman alimhutubu Trump, akisema kuwa kuiondoa Israel katika ajenda ya ziara yake ijayo ya Mashariki ya Kati, pamoja na mazungumzo yake na Hamas, Iran na al Houthi, ni ujumbe wa wazi kwamba Netanyahu hana ushawishi wowote kwa rais wa Marekani. Ameeleza kuwa kupuuzwa huko bila shaka kumemtia hofu Netanyahu na wenzake.
Thomas Friedman ameongeza kuwa, watu wa Israel bado wanajiona kama washirika wenye nguvu wa watu wa Marekani, na kinyume chake. Hata hivyo, ameongeza kuwa serikali ya sasa ya Netanyahu si mshirika wa kweli wa Marekani, kwani ni serikali ya kwanza katika historia ya Israel kuweka kipaumbele cha kutwaa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kuwafukuza Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na kujenga upya vitongoji vya walowezi, badala ya kufikia makubaliano ya amani na majirani zake wa Kiarabu.
Amesema kuwa Netanyahu amekataa matakwa ya Marekani kwa sababu Wayahudi wenye msimamo mkali katika serikali yake walitishia kuiondoa madarakani ikiwa atafanya hivyo. Amesema Netanyahu mwenyewe ana nia ya kushikilia madaraka yake, ambayo yanamhakikishia kinga ya kisiasa na kuchelewesha kesi za kisheria na kuepuka kifungo, akiweka mbele maslahi yake kuliko yale ya Marekani na hata Israel yenyewe.
342/
Your Comment